Tanzania ni moja ya nchi ambayo imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi sana ikiwemo milima. na hutumiwa hizo rasilimali ikiwemo na milima kuweza kuwa ni chanzo kikubwa chakuleta pato la nchi kupitia utalii wa ndani na nje ya nchi. miongoni mwa milima ambayo ni mikubwa na maarufu Tanzania ni Kilimanjaro, udzungwa, Usambara, Ol doinyo lengai na Rungwe. si hiyo ipo mingine mingi isipokuwa hiyo ni baadhi ya milima ambayo nimaarufu zaidi.
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani kutokana na mandhari nzuri ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote Afrika na inapatikana katika nchi ya Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini. Kilele cha Kibo
chenye urefu wa mita 5895 (futi 19340) ndio kivutio kikubwa kwa wageni
kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na kufunikwa na theluji.
Mlima huu ni moja kati ya milima ambayo kilele chake hufikiwa kwa
urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka kila
pande za dunia.
PICHA ZA MLIMA KILIMANJARO