Tanzania imebarikiwa kwa
wanyama wa kila aina. Kuna mbuga kubwa tatu ambazo Tanzania imehifadhi wanyama
mwitu. Mbuga hizi ni Mikumi, Manyara na Serengeti. Mbuga hizi zinatunzwa na wafanya
kazi wa wizara ya Utalii na Mali
Asili,Tanzania. Wageni wengi wanapendelea kuja Tanzania kutembelea mbuga za wanyama na hivyo kujionea fahari yetu katika mbuga hizo. Pia kupitia mbuga hizo husaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato la taifa na hivyo kuendeleza nchi yetu kujisaidia katika huduma zake mbalimbali.
Hifadhi ya Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikanandani ya hifadhi hii. Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.
Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa 3230 na ipo umbali wa kilometa 283 magharibi mwa Dar ea Salaam. Aidha hifadhi hii iko kaskazini ya mbuga ya Selouse na iko njiani unapoelekea katika hifadhi ya Udzungwa, Selouse na Ruaha kwa barabara kutoka Dar ea Salaam na Inapatikana katika Mkoa wa Morogoro.
Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la mbuga na misitu katika Tanzania ya kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na nchi ya Kenya.
Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara.
Kuna idadi kubwa ya wanyamapori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama, kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya zamadamu yalipatikana liko ndani ya Serengeti.
Twiga katika hifadhi ya mikumi |

Hifadhi ya Manyara ni maarufu sana nchini Tanzania kwa simba wanaopanda miti. aina hii
ya simba hupatikanandani ya hifadhi hii pekee barani Afrika.
Umaarufu
wa hifadhi ya Ziwa manyara unaongezeka kila siku kutokana na kukua kwa utalii wa
ndani ambapo wananchi wengi kutoka katika mikoa ya kaskazini mwa Tanzania
hupenda kutembelea hifadhi hii.
Hifadhi
hii ipo ndani ya Bonde la Ufa ambalo kingo zake zinaongeza mandhari
zaidi.Pundamilia katika hifadhi ya manyara |
Twiga wakiwa katika hifadhi ya mikumi |
Ukweli kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Kijiografia inapatikana katika Mkoa wa Mara. Kihistoria toka hapo zamani katika hifadhi hii ya Serengeti jamii ya Kabila la Wamaasai ambao ni jamii ya nilotiki ambayo kihistoria asilia yake ni Kusini mwa Sudani iliishi kwa miaka mingi pamoja na Wanyamapori katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba
kipindi cha wakati huo eneo hili la Serengeti ilikuwa
ikihusisha eneo linalofahamika leo hii kama Mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro ikijulikana kwa pamoja kama “Great Serengeti” kabla ya eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kutenganishwa mnamo mwaka wa 1959 na kupelekea jamii yote ya kabila la Wamaasai waliokuwa wakiishi eneo la Serengeti kuhamishiwa katika Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Asili ya jina Serengeti limetokana na lugha ya Kabila la Wamaasai lenye kumaanisha uwanda mpana.
- See more at: http://www.tazamaramanitanzania.com/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Serengeti.html#sthash.n6mChmIX.dpufSimba katika hifadhi ya Serengeti |
Mbega wakiwa katika hifadhi ya serengeti |
Ukweli kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Kijiografia inapatikana katika Mkoa wa Mara. Kihistoria toka hapo zamani katika hifadhi hii ya Serengeti jamii ya Kabila la Wamaasai ambao ni jamii ya nilotiki ambayo kihistoria asilia yake ni Kusini mwa Sudani iliishi kwa miaka mingi pamoja na Wanyamapori katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Kijiografia inapatikana katika Mkoa wa Mara. Kihistoria toka hapo zamani katika hifadhi hii ya Serengeti jamii ya Kabila la Wamaasai ambao ni jamii ya nilotiki ambayo kihistoria asilia yake ni Kusini mwa Sudani iliishi kwa miaka mingi pamoja na Wanyamapori katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba
kipindi cha wakati huo eneo hili la Serengeti ilikuwa
ikihusisha eneo linalofahamika leo hii kama Mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro ikijulikana kwa pamoja kama “Great Serengeti” kabla ya eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kutenganishwa mnamo mwaka wa 1959 na kupelekea jamii yote ya kabila la Wamaasai waliokuwa wakiishi eneo la Serengeti kuhamishiwa katika Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Asili ya jina Serengeti limetokana na lugha ya Kabila la Wamaasai lenye kumaanisha uwanda mpana.
- See more at: http://www.tazamaramanitanzania.com/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Serengeti.html#sthash.n6mChmIX.dpuf
Huyu mbega sio wa Serengeti labda Zanzibar.tafadhali toa maelezo yenye ukweli.utasababisha. udanganyifu mkubwa.
ReplyDelete