Zao la muhogo kwa wananchi walio wengi linachukuliwa kama la
kinga dhidi ya njaa. Miaka ya hivi karibuni kumezuka teknolojia nzuri ya
kufanya zao la muhogo litumike kwa usafi zaidi na hata kuwa zao la
biashara zaidi jambo ambalo litawafanya wakulima wa Tanzania kuwafikia
wakulima wa Afrika Magharibi ambao wameanza kusindika zao la muhogo kwa
muda mrefu na kunufaika kiuchumi.
Utafiti uliofanyika nchini Italia kuhusiana na zao hilo unaonyesha kuwa muhogo unaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali zaidi ya 300 yakiwemo unga wa muhogo, tambi, biskuti, mafuta ya lishe, keki, sabuni ya
unga, kuni, mboga, pamoja na bidhaa nyingine nyingi.
![]() |
| Zao la muhogo |

Maofisa ugani wakieneza elimu ya kisasa ya
kusindika muhogo katika maeneo mengi nchini miaka kumi ijayo, zao la
muhogo litakuwa ni zao kubwa na lenye heshima katika kuinua uchumi na
kipato cha mkulima kwa kulifanya kuwa zao la chakula na biashara.