Alitoa
kauli hiyo jana jioni wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya
Kiwere, baada ya kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za
walimu kwenye Shule ya Sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani
Iringa.
Waziri
Mkuu alisema walimu hao
watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji yaliyokwishawasilishwa na watakapopata mgawo wao, hawana budi kuangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo.
watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji yaliyokwishawasilishwa na watakapopata mgawo wao, hawana budi kuangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo.
Akifafanua kuhusu kasi ya ujenzi wa maabara, Waziri Mkuu alisema: “Mkoa mzima wa Iringa unahitaji maabara 318 na zilizo tayari mpaka sasa ni 108.
“Lakini
kuna nyingine 141 ambazo zimekwishaanza kujengwa na zimefikia hatua
nzuri. Nimeambiwa katika muda mfupi ujao kutakuwa na maabara 249
zilizokamilika,” alisema.
zilizokamilika,” alisema.
“RC
inabidi uwasukume watu wako ili hizi 69 ambazo hazijaanza kujengwa
zikamilike kabla ya Juni mwaka huu kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete
alivyoelekeza. Alisema hataongeza tena muda wa ujenzi,” aliongeza.
Alisema
elimu ni sekta ya msingi ambayo Serikali imeamua kuipa umuhimu wa
kipekee na kuiweka katika moja ya maeneo sita muhimu ya kipaumbele chini
ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN).
Waziri Mkuu aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii na wawe wasikivu, ili wafanye vizuri zaidi kwenye masomo yao.
Mapema,
akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Ofisa Elimu wa Wilaya ya Iringa,
Leonard Msigwa, alisema ujenzi wa nyumba hizo nne zenye pande mbili,
umegharimu Sh milioni 323.2.
Alisema nyumba hizo zenye vyumba vitatu vya kulala, sebule na jiko, zina uwezo wa kubeba familia nane.
Msigwa
alisema ujenzi wa nyumba hizo ulifanywa na shirika la Deswos la
Ujerumani kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na
wananchi.
Pia
walisaidiwa kujengewa tangi la maji na mabweni mawili yenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi 112 kila moja kwa ajili ya wasichana.
Akifafanua
kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, Ofisa Elimu huyo alisema hadi sasa
wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya Kemia na Bayoolojia, lakini
bado viko kwenye hatua ya kupaka rangi. Aidha mfumo wa gesi na maji
umekwishafungwa ndani ya vyumba vya maabara.
“Ujenzi
wa maabara hadi sasa umekwisha gharimu Sh milioni 52.8/- na kwa
Februari 2015, tumefanikiwa kutengeneza baadhi ya samani za maabara
yaani meza 24 na stuli 96 zenye thamani ya Sh milioni 8.9,” alisema.
No comments:
Post a Comment