Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwataarifu
wananchi kuwa limeongeza muda wa kutuma maombi ya Mafunzo ya Stashahada
ya Ualimu, awamu ya pili
hadi tarehe 28 Februari 2015.
Baada ya tarehe hiyo, majina ya waombaji watakaochaguliwa kujiunga na
mafunzo ya Stashahada ya Ualimu awamu ya pili yatatangazwa mwanzoni mwa
mwezi Machi 2015 kwenye tovuti ya Baraza ambayo inaonekana katika
Tangazo hili.
Watu wote wenye sifa za kujiunga na mafunzo haya wanaombwa kuitumia
fursa hii muhimu kama inavyoelekezwa kwenye tovuti ya Baraza: Kwa maelezo zaidi
bofya hapa.
Imetolewa na;
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Tarehe 10/2/2015
No comments:
Post a Comment