Sunday 22 February 2015

JE WAJUA HILI?... AU NDO WAJUZWA?

Ivi waijua korosho au waisikia? .....Watumia sana lakini ni baada ya kuikuta dukani imeshakwisha andaliwa....je, watambua mwanzo kabla ya kutengeneza na kuweka dukani teali kwa matumizi inafananaje?....
OOOOOOhhhh...sikia fahari leo hii kutambua kabla ya kuitumia hiyo korosho inatoka wapi..kwani ninahofu kwako,kuweza tu kuitamka na kuitumia pasina kutambua vipi inakuwa mwanzo kabla ya kukufikia.
Sasa kabla bado korosho haijawa korosho kutoka katika miti yake huanza kufanyiwa maandalizi ya mashamba ambayo miti hiyo hulimwa, na maandalizi hayo huanza tuu baada kuanza kutokeza maua ya zao hilo.
Mti wa mkorosho


Miti hii mpaka kufikia hatua ya kuzaa korosho huwa ina fanyiwa kharama mbalimbali kama kulimiwa na kupuliziwa dawa zaidi ya mara tatu na zaidi katika kipindi tofauti tofauti.

Baada ya maandalizi hayo huwa inasubiriwa kwakipindi fulani wakati huo kukiwa na maangalizi ya hali ya juu zidi ya wadudu waaribio maua ya korosho,

Ndipo baadae baada ya uangalizi na huduma mbalimbali huanza taratibu kutengeneza korosho mbichi ( ambazo huitwa madafu ya korosho),matunda (mabibo ya korosho) hatimaye kukauka na kuanza kuanguka kutoka mtini. ikifika hatua hyo sasa ndipo wakulima huanza kuokota korosho na kurudisha

Saturday 21 February 2015

TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KUTUMA MAOMBI YA MAFUNZO YA STASHAHADA YA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2015

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi  (NACTE) linapenda kuwataarifu wananchi kuwa limeongeza muda wa kutuma maombi ya Mafunzo ya Stashahada ya Ualimu, awamu ya pili hadi tarehe 28 Februari  2015. Baada ya tarehe hiyo, majina ya waombaji watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Stashahada ya Ualimu awamu ya pili yatatangazwa mwanzoni mwa mwezi Machi 2015 kwenye tovuti ya Baraza ambayo inaonekana katika Tangazo hili.
Watu wote wenye sifa za kujiunga na mafunzo haya wanaombwa kuitumia fursa hii muhimu kama inavyoelekezwa kwenye tovuti ya Baraza:  Kwa maelezo zaidi bofya hapa.


Imetolewa na;

Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Tarehe 10/2/2015

SERIKALI YAAHIDI KUAJILI WALIMUU WAPYA 35,000 MWAKA HUU

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema Serikali imepanga kuajiri walimu zaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari, ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu nchini.
Alitoa kauli hiyo jana jioni wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere, baada ya kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenye Shule ya Sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa.

 
Waziri Mkuu alisema walimu hao
watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji yaliyokwishawasilishwa na   watakapopata mgawo wao, hawana budi kuangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo.
Akifafanua kuhusu kasi ya ujenzi wa maabara, Waziri Mkuu alisema: “Mkoa mzima wa Iringa unahitaji maabara 318 na zilizo tayari mpaka sasa ni 108.
 
“Lakini kuna nyingine 141 ambazo zimekwishaanza kujengwa na zimefikia hatua nzuri. Nimeambiwa katika muda mfupi ujao kutakuwa na maabara 249

KUMBUKUMBU ZA VURUGU ZA GESI MTWARA


Hiki kilikua ni kipindi cha majonzi makubwa kwa wana mtwara katika sakata la kuhitaji haki yao. Ama hakika kwa wale wote tunaokumbuka kipindi hiki hatutamani kuhitajia kutokea tena kipindi kama hiki. Simanzi zilitawala kutokana na watu kuaribiwa makazi yao, na hata kukosa ndugu zao.Mungu awatakie kheri wote waliokakumbwa na kharika lile.

Zifuatazo ni baadhi ya picha ambazo huonyesha matukio mbalimbali ya kipindi kile:-

ONA FAHARI KUSINI YETU

Pande za kusini Tanzania inawakilishwa na mikoa ya Mtwara,Lindi na Ruvuma ikipakana na mikoa ya Nyanda za juu Kusini ambayo ni Mbeya, Iringa na Njombe . Hii ni mikoa maarufu ambayo hufahamika. Huwa inajipatia umaarufu sana  hususani katika kilimo kikubwa sana cha Biashara Tanzania cha Korosho, Kupitia kilimo hicho kimekua kikipatia pato serikali na hata kuwawezesha wanainchi waishio pande hizo kuendeshea maisha yao.

Hapa chini ni muonekano wa picha za Korosho na Mabibo yake.

Korosho na matunda yake.

Korosho zikiwa juu ya mti wake.
Hivi ndivyo ambavyo twajivunia nyumbani Kusini. Pamoja na shughuli si moja tuu. kuna nyingi na nyingi,miongoni mwa hizo ni shughuli za uvuvi ambazo hufanyika katika bahari ya Hindi, Pia kilimo cha Mahindi,Mihogo na hata Mtama. Hivy vyote hupatikana Maeneo haya ya kusini.

Pia Mikoa yetu hii imejaliwa kuwa na bandari kubwa miongoni mwa bandari zipatikanazo Tanzania, Na hata selous  ambayo hiyo hupatikana Liwale-lindi ikipakana na Mkoa wa Morogoro.
Pia ni fahari kwetu kutokana