Thursday 7 May 2015

TAMBUA MBUGA KUU TATU ZA WANYAMA TANZANIA

Tanzania imebarikiwa kwa wanyama wa kila aina. Kuna mbuga kubwa tatu ambazo Tanzania imehifadhi wanyama mwitu. Mbuga hizi ni Mikumi, Manyara na Serengeti. Mbuga hizi zinatunzwa na wafanya kazi wa wizara ya Utalii na Mali Asili,Tanzania. Wageni wengi wanapendelea kuja Tanzania kutembelea mbuga za wanyama na hivyo kujionea fahari yetu katika mbuga hizo. Pia kupitia mbuga hizo husaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato la taifa na hivyo kuendeleza nchi yetu kujisaidia katika huduma zake mbalimbali.

Hifadhi ya Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikanandani ya hifadhi hii. Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.
Twiga katika hifadhi ya mikumi

Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa 3230 na ipo umbali wa kilometa 283 magharibi mwa Dar ea Salaam. Aidha hifadhi hii iko kaskazini ya mbuga ya Selouse na iko njiani unapoelekea katika hifadhi ya Udzungwa, Selouse na Ruaha kwa barabara kutoka Dar ea Salaam na Inapatikana katika Mkoa wa Morogoro.

Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la mbuga na misitu katika Tanzania ya kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na nchi ya Kenya.
Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara.
Kuna idadi kubwa ya wanyamapori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama, kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.

Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya zamadamu yalipatikana liko ndani ya Serengeti.

Hifadhi ya Manyara ni maarufu sana nchini Tanzania kwa simba wanaopanda miti. aina hii ya simba hupatikanandani ya hifadhi hii pekee barani Afrika.
Umaarufu wa hifadhi ya Ziwa manyara unaongezeka kila siku kutokana na kukua kwa utalii wa ndani ambapo wananchi wengi kutoka katika mikoa ya kaskazini mwa Tanzania hupenda kutembelea hifadhi hii. Hifadhi hii ipo ndani ya Bonde la Ufa ambalo kingo zake zinaongeza mandhari zaidi.
Pundamilia katika hifadhi ya manyara

Twiga wakiwa katika hifadhi ya mikumi

Ukweli kuhusu  Hifadhi ya Taifa  ya Serengeti
Hifadhi  ya Taifa  ya Serengeti  Kijiografia  inapatikana  katika  Mkoa wa Mara.  Kihistoria  toka  hapo zamani  katika  hifadhi hii ya Serengeti jamii ya Kabila la Wamaasai ambao  ni jamii ya nilotiki  ambayo  kihistoria  asilia  yake  ni  Kusini  mwa  Sudani  iliishi  kwa miaka  mingi  pamoja na Wanyamapori  katika  hifadhi  ya Taifa  ya Serengeti.
        Ikumbukwe  na ieleweke  ya kwamba  kipindi  cha wakati  huo eneo  hili la Serengeti  ilikuwa  ikihusisha eneo  linalofahamika leo  hii  kama Mamlaka  ya hifadhi ya Ngorongoro ikijulikana  kwa pamoja  kama “Great  Serengeti” kabla ya  eneo  la mamlaka ya hifadhi  ya Ngorongoro  kutenganishwa  mnamo  mwaka  wa 1959 na  kupelekea  jamii  yote ya  kabila la Wamaasai waliokuwa  wakiishi  eneo la Serengeti  kuhamishiwa  katika  Mamlaka ya hifadhi  ya Ngorongoro.
        Asili ya jina Serengeti limetokana na lugha ya Kabila la Wamaasai lenye  kumaanisha  uwanda  mpana.
- See more at: http://www.tazamaramanitanzania.com/Hifadhi%20ya%20Taifa%20ya%20Serengeti.html#sthash.n6mChmIX.dpuf

Simba katika hifadhi ya Serengeti

Mbega wakiwa katika hifadhi ya serengeti

1 comment:

  1. Huyu mbega sio wa Serengeti labda Zanzibar.tafadhali toa maelezo yenye ukweli.utasababisha. udanganyifu mkubwa.

    ReplyDelete