Sunday 22 February 2015

JE WAJUA HILI?... AU NDO WAJUZWA?

Ivi waijua korosho au waisikia? .....Watumia sana lakini ni baada ya kuikuta dukani imeshakwisha andaliwa....je, watambua mwanzo kabla ya kutengeneza na kuweka dukani teali kwa matumizi inafananaje?....
OOOOOOhhhh...sikia fahari leo hii kutambua kabla ya kuitumia hiyo korosho inatoka wapi..kwani ninahofu kwako,kuweza tu kuitamka na kuitumia pasina kutambua vipi inakuwa mwanzo kabla ya kukufikia.
Sasa kabla bado korosho haijawa korosho kutoka katika miti yake huanza kufanyiwa maandalizi ya mashamba ambayo miti hiyo hulimwa, na maandalizi hayo huanza tuu baada kuanza kutokeza maua ya zao hilo.
Mti wa mkorosho


Miti hii mpaka kufikia hatua ya kuzaa korosho huwa ina fanyiwa kharama mbalimbali kama kulimiwa na kupuliziwa dawa zaidi ya mara tatu na zaidi katika kipindi tofauti tofauti.

Baada ya maandalizi hayo huwa inasubiriwa kwakipindi fulani wakati huo kukiwa na maangalizi ya hali ya juu zidi ya wadudu waaribio maua ya korosho,

Ndipo baadae baada ya uangalizi na huduma mbalimbali huanza taratibu kutengeneza korosho mbichi ( ambazo huitwa madafu ya korosho),matunda (mabibo ya korosho) hatimaye kukauka na kuanza kuanguka kutoka mtini. ikifika hatua hyo sasa ndipo wakulima huanza kuokota korosho na kurudisha
nyumbani teali kwa kuandaa kwa kuuza.

hizi picha hapa chini zinaonesha korosho zikiwa bado hazijaandaliwa kwa matumizi ya kula na baada ya kuandaliwa kwa ajili ya kula.



No comments:

Post a Comment