Saturday 21 February 2015

ONA FAHARI KUSINI YETU

Pande za kusini Tanzania inawakilishwa na mikoa ya Mtwara,Lindi na Ruvuma ikipakana na mikoa ya Nyanda za juu Kusini ambayo ni Mbeya, Iringa na Njombe . Hii ni mikoa maarufu ambayo hufahamika. Huwa inajipatia umaarufu sana  hususani katika kilimo kikubwa sana cha Biashara Tanzania cha Korosho, Kupitia kilimo hicho kimekua kikipatia pato serikali na hata kuwawezesha wanainchi waishio pande hizo kuendeshea maisha yao.

Hapa chini ni muonekano wa picha za Korosho na Mabibo yake.

Korosho na matunda yake.

Korosho zikiwa juu ya mti wake.
Hivi ndivyo ambavyo twajivunia nyumbani Kusini. Pamoja na shughuli si moja tuu. kuna nyingi na nyingi,miongoni mwa hizo ni shughuli za uvuvi ambazo hufanyika katika bahari ya Hindi, Pia kilimo cha Mahindi,Mihogo na hata Mtama. Hivy vyote hupatikana Maeneo haya ya kusini.

Pia Mikoa yetu hii imejaliwa kuwa na bandari kubwa miongoni mwa bandari zipatikanazo Tanzania, Na hata selous  ambayo hiyo hupatikana Liwale-lindi ikipakana na Mkoa wa Morogoro.
Pia ni fahari kwetu kutokana
na kuwa na gesi ambayo huzalishwa kwa kiwango kikubwa nchini na kusaidia baadhi ya maeneo ikihusishwa kusini yenyewe.
Hivyo ni fahari kwa wana kusini, na nifaraja kubwa kwetu kutokana na vitu hivyo.

No comments:

Post a Comment