Wednesday 13 May 2015

MILIMA MAARUFU TANZANIA.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi sana ikiwemo milima. na hutumiwa hizo rasilimali ikiwemo na milima kuweza kuwa ni chanzo kikubwa chakuleta pato la nchi kupitia utalii wa ndani na nje ya nchi. miongoni mwa milima ambayo ni mikubwa na maarufu Tanzania ni Kilimanjaro, udzungwa, Usambara, Ol doinyo lengai na Rungwe. si hiyo ipo mingine mingi isipokuwa hiyo ni baadhi ya milima ambayo nimaarufu zaidi.

Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani kutokana na mandhari nzuri ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote Afrika na inapatikana katika nchi ya Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini. Kilele cha Kibo chenye urefu wa mita 5895 (futi 19340) ndio kivutio kikubwa kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na kufunikwa na theluji.
Mlima huu ni moja kati ya milima ambayo kilele chake hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka kila pande za dunia.

                        PICHA ZA MLIMA KILIMANJARO
 

















Milima ya udzungwa ni jina la hifadhi inayopatikana katika nchi ya Tanzania na jina hili limetookana na milima hiyo ya udzungwa ambayo ndani yake ni makazi ya wanyama pori wa aina mbalimbali. Ina ukubwa wa kilometa 1990, na ni hifadhi yenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambazo hazipatikani katika sehemu nyingine duniani.
hifadhi iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65 kutoka katika Hifadhi ya
Mikumi.
Kati ya aina sita za jamii ya nyani wanaopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katik hifadhi hii pekee; Mbega Mwekundu, wa Iringa(Iringa red colobus monkey) na "Sanje Crested mangabey" ambaye alikuwa hajulikani mpaka mwaka 1979.

Milima ya Usambara ni sehemu iliyoinuka upande wa Kaskasini Mashariki wa nchi ya Tanzania. Milima ya usambara ni milima kunjamano yaani milima iliyoshikana kutoka mlima mmoja mpaka mwingine. Wenyeji wanaoishi maeneo haya ni Wasambaa, ndiyo maana ikaitwa milima ya usambara. Iko mkoa wa Tanga kuanzia Korongwe kuelekea kaskazini mpaka inapakana na milima ya upare.

Ol Doinyo Lengai (Kimaasai "mlima wa Mungu") ni mlima wa volkeno katika Tanzania ya Kaskazini. Iko takriban 120 km kaskazini-magharibi ya Arusha. Iko 25 km kusini ya Ziwa la Magadi (Tanzania - "Lake Natron").
Jina la mlima ni Kimaasai lamaanisha "mlima wa Mungu". Mlima una kimo cha 2690 m juu ya UB. Ni volkeno ya pekee duniani kutokana na aina ya lava yake inayotoka hali ya kiowevu (majimaji) lakini si moto sana (mnamo 500° - 600 °C).
Ol Doinyo Lengai ililipuka tena Machi 2006. Katika mwaka 2007 mlima umesababisha mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara kuanzia 12 Julai. Tetemeko la 18 Julai lilisikika hadi Nairobi.

Mlima wa Rungwe ni volkeno iliyozimika ya Tanzania kusini magharibi ikikadiriwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka 2000 hadi 5000 iliyopita. Ukiwa na kimo cha 2960 m ni mlima mkubwa wa Tanzania ya Kusini.
Mlima unasimama juu ya ncha ya kaskazini ya Ziwa Nyasa. Upande wa kusini-mashariki wa mlima hupokea usimbishaji wa 3,000 mm kwa mwaka ambao ni juu kabisa katika Tanzania.
Mazingira ya mlima ni nchi yenye rutba na kilimo. Rungwe ni eneo la Wanyakyusa.
Jina la mlima limekuwa pia jina la wilaya ya Rungwe.


 

No comments:

Post a Comment