Wednesday 13 May 2015

MILIMA MAARUFU TANZANIA.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi sana ikiwemo milima. na hutumiwa hizo rasilimali ikiwemo na milima kuweza kuwa ni chanzo kikubwa chakuleta pato la nchi kupitia utalii wa ndani na nje ya nchi. miongoni mwa milima ambayo ni mikubwa na maarufu Tanzania ni Kilimanjaro, udzungwa, Usambara, Ol doinyo lengai na Rungwe. si hiyo ipo mingine mingi isipokuwa hiyo ni baadhi ya milima ambayo nimaarufu zaidi.

Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani kutokana na mandhari nzuri ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote Afrika na inapatikana katika nchi ya Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini. Kilele cha Kibo chenye urefu wa mita 5895 (futi 19340) ndio kivutio kikubwa kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na kufunikwa na theluji.
Mlima huu ni moja kati ya milima ambayo kilele chake hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka kila pande za dunia.

                        PICHA ZA MLIMA KILIMANJARO
 

Saturday 9 May 2015

SHERIA YA MAKOSA YA MITANDAO,2015

Sheria hii ya makosa ya mtandao, 2015 imebainika kuwa na mapungufu makubwa sana. Mapungufu hayo yamebainika kuwa, kama sheria ikipita yanaweza kuifanya nchi ikawa ni kati nchi adui za matumizi ya mtandao wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano duniani.

Watanzania wote wanatakiwa kufahamu kuwa muswada ukipita utatumika nchini kote yani Tanzania Bara na Visiwani. Watanzania waliowengi hawafahamu Sheria hii inawahusu kwa namna gani; lakini kwa lugha rahisi ni kuwa itamuathiri mtu yeyote anayeweza tumia mtandao wa intaneti kwa kutimia kifaa chochote iwe kompyuta kubwa au vifaa vyenye uwezo wa kufanya kazi kama kompyuta kama Simu za mikononi,saa, televisheni na vifaa vingine vinavyoendana na hivyo.
                                                                               :ZAIDI SOMA HAPA:

Thursday 7 May 2015

TAMBUA MBUGA KUU TATU ZA WANYAMA TANZANIA

Tanzania imebarikiwa kwa wanyama wa kila aina. Kuna mbuga kubwa tatu ambazo Tanzania imehifadhi wanyama mwitu. Mbuga hizi ni Mikumi, Manyara na Serengeti. Mbuga hizi zinatunzwa na wafanya kazi wa wizara ya Utalii na Mali Asili,Tanzania. Wageni wengi wanapendelea kuja Tanzania kutembelea mbuga za wanyama na hivyo kujionea fahari yetu katika mbuga hizo. Pia kupitia mbuga hizo husaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato la taifa na hivyo kuendeleza nchi yetu kujisaidia katika huduma zake mbalimbali.

Hifadhi ya Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikanandani ya hifadhi hii. Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.
Twiga katika hifadhi ya mikumi

Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa 3230 na ipo umbali wa kilometa 283 magharibi mwa Dar ea Salaam. Aidha hifadhi hii iko kaskazini ya mbuga ya Selouse na iko njiani unapoelekea katika hifadhi ya Udzungwa, Selouse na Ruaha kwa barabara kutoka Dar ea Salaam na Inapatikana katika Mkoa wa Morogoro.

Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la mbuga na misitu katika Tanzania ya kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na nchi ya Kenya.
Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara.
Kuna idadi kubwa ya wanyamapori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama, kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.

JUA FAIDA YA ZAO LA MUHOGO KIUCHUMI

Zao la muhogo kwa wananchi walio wengi linachukuliwa kama la kinga dhidi ya njaa. Miaka ya hivi karibuni kumezuka teknolojia nzuri ya kufanya zao la muhogo litumike kwa usafi zaidi na hata kuwa zao la biashara zaidi jambo ambalo litawafanya wakulima wa Tanzania kuwafikia
Zao la muhogo
wakulima wa Afrika Magharibi ambao wameanza kusindika zao la muhogo kwa muda mrefu na kunufaika kiuchumi.
Utafiti uliofanyika nchini Italia kuhusiana na zao hilo unaonyesha kuwa muhogo unaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali zaidi ya 300 yakiwemo unga wa muhogo, tambi, biskuti, mafuta ya lishe, keki, sabuni ya
unga, kuni, mboga, pamoja na bidhaa nyingine nyingi.
Maofisa ugani wakieneza elimu ya kisasa ya kusindika muhogo katika maeneo mengi nchini miaka kumi ijayo, zao la muhogo litakuwa ni zao kubwa na lenye heshima katika kuinua uchumi na kipato cha mkulima kwa kulifanya kuwa zao la chakula na biashara.